Thursday, March 19, 2009

SKENDO KUTOKA GLOBAL PUBLISHER

Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba, mademu wengi wamekuwa wakiingia mkenge kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii hatimaye kupachikwa ujauzito na kuachwa solemba.

Miongoni mwa akinadada waliokumbwa na adha hiyo ni Jamila Mbwana aliyezalishwa kisha kutelekezwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Mheshimiwa Temba.

Jamila alisema kuwa, awali uhusiano wake na msanii huyo ulikuwa bomba, lakini baada ya kuzalishwa penzi lilipungua ambapo ‘mchizi’ aliamua kumwaga na kumuoa msichana mwingine.

“Achilia mbali suala la kuniacha na kuoa mwanamke mwingine, lakini kimsingi amekuwa hamlei mwane ipasavyo, kwa asilimia kubwa nimekuwa nikimlea mtoto mwenyewe,” anaeleza Jamila.

Hata hivyo, Temba ambaye sasa hivi ameoa mwanamke mwingine mara kwa mara amekuwa akikanusha kumtelekeza mtoto wake na kueleza kuwa, bado anaendelea kumhudumia.

Mwingine ni msanii wa zamani wa Kaole aitwaye Lilian ambaye amezalishwa na msanii mwenzake Tuesday Kihangala kabla ya kutelekezwa na kula msoto na mwanae.

Lilian pia analalamikia msaada mdogo anaoupata kutoka kwa Chuzi ambaye sasa hivi anajulikana kama ‘mzee wa totoz’.

Msanii Aboubakar Katwila ‘Q-Chiller’ naye anadaiwa kumtelekeza mtoto wake aliyezaa na binti aitwaye Shaha Juma.

Shaha katika mahojiano na gazeti hili alieleza kuwa, mzazi mwezake huyo amekuwa akisuasua katika kumpatia mahitaji muhimu mtoto wake huku akidaiwa kujiachia na mwanamke mwingine nchini Kenya.

Q-Chiller hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia shutuma hizo kwani kwasasa yuko nhini Kenya kwa shughuli zake za kimuziki.

Wengine wanaodaiwa kutelekeza watoto wao ni pamoja na msanii Mohammed Mwikogi ‘Frank’ aliyezaa na binti aliyetajwa kwa jina moja la Amina, mwanasoka Mrisho Ngassa anayedaiwa kumtelekeza mkewe na mtoto huko Mwanza na kuoa mwanamke mwingine.

Hata hivyo, sababu za baadhi ya mastaa kuwapa ujauzito mabinti kisha kuwaacha zimetajwa kuchangiwa na umaarufu ambapo wahusika hufikia kipindi cha kuwaona ‘malava’ wao wa nyuma kama ‘zilipendwa’.

Akiongea na Gazeti hili mmoja wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Aisha Mzee, ambaye binti yake alizalishwa na kutelekezwa na msanii wa filamu (Jina kapuni) alisema kuwa, wengi wa wasanii hao huanzisha uhusiano na mabinti wa watu kwa ahadi ya kuwaoa, lakini umaarufu unapoongezeka, huwaacha solemba na kuoa wanawake wengine.

“Binti yangu kama unavyomuona amekuwa na msanii yule tangu unaanza mambo ya uigizaji, enzi hizo alikuwa hata kuvaa hajui lakini sasa hivi amekuwa maarufu anaona hastahili kuwa na msichana kama mwanangu.

“Kibaya zaidi ni kwamba amemtelekeza baada ya kumzalisha na sasa anapata tabu na mtoto, mimi namuachia Mungu,”alisema mama huyo.

Aidha, mama huyo aliwatahadharisha wasichana kuwa makini na hawa wanaojiita wasanii kwani wengi wao ni waongo, matapeli wa mapenzi na wachafuzi wanaoweza kuyaharibu maisha yao.

Kama umetelekezwa na Supastaa, kigogo yeyote au unamjua staa aliyetelekeza mtoto cheki na sisi kwa no 0716-007373- 0755261367

Post a Comment
Truck Driving Schools
Idadi ya Watu