Saturday, December 3, 2011

ILIVYOKUWA 'LIVE' KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 12 YA CLOUDS FM REDIO

 
 Keki.
Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto) wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa kampuni ya Prime Time Promotions Juhayna Ajmy Kusaga katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto) wakimsikiliza mtangazaji mwenzao Regina Mwalekwa wakiti walipomfanyia 'suprise' ya kumletea mke wa Ephraim Kibonde studio bila yeye kujua.
 Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto) wakimsikiliza Mbunge wa Ubungo, jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Chadema, John Mnyika wakati akihojiwa katika maadhimisho ya miaka 12 ya Clouds Fm.
 Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka aitia msisitizo.
 Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka akimlisha keki mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo.
 Mtangazaji wa Clouds Fm kipindi cha Njia Panda Dokta Isack Maro akifanyiwa  mahojiano na Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto).
 Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Amprifaya, Millard Ayo (kati) akieleza kwa kina katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
 Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, akiongea na watangazaji wenzake wa kipindi cha Sports Extra Alex Mwambano na Shafii Dauda (kati) katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde (wa pili kushoto) akitilia msisitizo jambo wakati akiwa na Mkurugenzi wa Msama Promotions Bw. Alex Msama. Wengine ni Watangazaji wa Clouds TV Ceaser Daniel na Sophia Kessy.
Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde akiwa na mkewe.
Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto) wakifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Amprifaya, Millard Ayo akisoma taarifa ya habari ndani ya Clouds TV katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Ephraim Kibonde (kushoto) akitambulisha baadhi ya wanakikosi cha Idara ya Habari ya Clouds Fm ambaye ni Joyce Shebe, Philip Mwihava pamoja na Austine.


Watangazaji wa Clouds Fm katika kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia) na Ephraim Kibonde (kushoto) wakifanya mahojiano na katibu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akicharaza gitaa katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
Watangazaji wa Clouds Fm kutoka kushoto ni Hamis Mandi a.k.a B12 pamoja na Fatuma Hasan a.k.a Dj Fetty wakiongea na Mkurugenzi wa Utafiti wa Clouds Fm Ruge Mutahaba.
Muasisi wa wa muziki wa hip hop Zavala (kulia), akifafanua jambo wakati wa mahojiano na
Meneja wa Wanaume TMK Said Fela a.k.a Mkubwa na wanawe akifafanua jambo wakati akihojiwa.
Mtangazaji wa Clouds Fm Fatuma Hasan a.k.a Dj Fetty akiongea na mwanamuziki AT katikati ni muasisi wa muziki wa hip hop Zavala akifuatiliwa kwa karibu maongezi.
'Naongea na Liziwani..wewe Liziwani lipoti hizo ufikisheeeee...huyo ni Izo Business akiachia vitu huku akifuatiliwa kwa karibu na muasisi wa muziki wa hip hop Zavala pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm Fatuma Hasan a.k.a Dj Fetty.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA Yustus Mkinga (kulia) akifafanua jambo wakati akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Clouds Fm Hamis Mandi a.k.a B12 pembeni yake ni Mbunge wa Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr. Hamisi Kigwangalla.
Watangazaji wa Clouds Fm kutoka kulia ni Ruben Ndege, Adamu Mchomvu, Hamis Mandi a.k.a B12 pamoja na Fatuma Hasan a.k.a Dj Fetty wakionyesha alama ya C kuashiria kuwa ni Clouds Fm, Choice Fm na Coconut Fm redio zote hizo zinamilikiwa na Clouds Media Group katika maadhimisho hayo ya miaka 12 ya Clouds Fm yaliyofanyia jana Dar es Salaam.
---
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw. SAID MECK SADICK alipongeza Clouds FM kwa kutimiza miaka 12 tangu kuanzishwa kwake na kufanikiwa kuteka soko la vijana ikiwemo kuwapatia ajira na elimu kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na kituo hiki.

Akizungumza katika kipindi cha Power Break Fast ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 12 ya Clouds FM, Mkuu huyo wa mkoa alsema kituo hiki kinapaswa kuongeza idadi ya vipindi vya kuelimisha vijana kuwa wajasiliamali kwa lengo la kuachana na utegemezi na kupunguza idadi ya vijana wasiokuwa na kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema katika Jiji la Dar es Salaam kumekuwa na kiwango kikubwa cha uvunjaji wa sheria ambao umekuwa ukidhibitiwa wavunjaji hao wa sheria hutoa vitisho vya kuandamana au kulala barabarani jambo ambalo limekuwa likifanyiwa kazi na Serikali ili kudhibitiwa.

Kuhusiana na ongezeko kubwa la watu wanaoingia na kuishi Dar es Salaam kutoka mikoani mkuu huyo wa mkoa alisema watu hao wanapaswa kufuata sheria zilizopo ikiwemo za kufanya biashara katika maeneo maalum yaliyotengwa na Jiji badala ya kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

2 comments :

comfort joely said...

clouds mko juu!!

Anonymous said...

clouds mko juu!!!

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu