Baadhi ya waumini wa Kiislam walifanya ibada ya kusalia maiti ya Marehemu Mzee Said Fundi maarufu kwa jina la Mzee Kipara aliyefariki dunia jana Maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam.

Na Francis Dande
Maelfu ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam na vitongoji vyake, leo wamejitokeza katika mazishi ya msaanii mkongwe wa sanaa ya maigizo, Fundi Said maarufu kama mzee Kipara.

Mazishi hayo yalifanyika jioni ya leo katika makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Waziri wa Afrika Mashariki, Mh. Samuel Sitta na viongozi wengine akiwemo mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemens pamoja na wasanii mbalimbali.

Baadhi ya Wasafii na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Mzee Kipara wakati wa kuelekea Makaburi ya Kigogo Jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Sehemu ya Umati uliojitokeza kwa wingi kumzika Mzee Kipara ukielekea yalipo Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Mpiga Picha wa Globu ya Jamii, Francis Dande akiwa na Muigizaji wa Sanaa ya Maigizo wa siku nyingi, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small walipokutana kwenye maziko ya Marehemu Mzee Kipara kwenye Makaburi ya Kigogo jijini Dar es Salaam leo. Picha/Habari na Michuzi Blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: