Wednesday, May 29, 2013

RAMBI RAMBI YA KIFO CHA MAREHEMU MANGWER TOKA CHAMA CHA MUZIKI WAKIZAZI KIPYA TANZANIA (TUMA)

Chama cha muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania (TUMA), kimepokeakwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa mwanamuzikimaarufu na mashuhuri nchini Albert Mangwea (Ngwair) aliyefariki jijiniJohannesburg nchini Afrika Kusini jana.

Mwenyekiti wa TUMA nchini, Fredrick G Mariki (Mkoloni) ametoasalamu hizo za pole kwa familia ya marehemu Mangwea, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wa Bongo Fleva waliopo ndani na nje yanchi kutokana na kuondokewa kwa msanii maarufu Albert Mangwair.

Marehemu Albert Mangwea ambaye alikuwa nchini Afrika Kusini kwashughuli za kimuziki alifikwa na mauti hayo huku akiwa amelala katika chumba ambacho alikuwa na rafiki yake aliyetambulika kwa jina la M to The P ambaye naye alikimbizwa Hospitali ya St Helen ilityopo nchiniAfrika Kusini kwa matibabu huku taarifa kamili ya kilichosababisha kifo cha Mangwea kikiwa bado hakijajulikana mpaka hapo Hospitali hiyoitakaposema.

“kwa niaba ya wanachama wa TUMA na Watanzania wote kwa ujumlanapenda kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu AlbertMangwair kutokana na pigo hili kubwa na kwa kweli tumepoteza msaniiwa kizazi kipya ambaye Taifa lilikuwa likijivunia kuwepo kwake nakazi zake” alisema Mkoloni.

Chama cha TUMA kinaungana na Watanzania wote katika kipindi hikikigumu na kinatoa ushirikiano wa hali na mali kama ambavyokimekuwa kikifanya hivyo katika mambo mengine yanayohusu wasaniinchini.

Mkoloni alimaliza kwa kusema kuwa “ni kweli tulimpenda lakiniMungu alimpenda zaidi na kuongeza kuwa ni wakati mgumu natunatakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kipindi hiki huku akitoaangalizo kwa watu wanaotaka kutumia fursa hii kwa ajili ya maslahi yaobinafsi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu