Saturday, October 3, 2015

DK MAGUFULI, CHILOLO WAISAMBARATISHA NGOME YA TUNDU LISSU SINGIDA MASHARIKI

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi katika Jimbo la Manyoni, mkoani Singida, wakati wa mkutano wa kampeni. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali kwa wananchi kuhusu elimu ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, utaratibu utakaoanza mwakani endapo wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza nchi.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiombewa dua na Imamu wa Msikiti wa Puma,Ramadhan Khamis Jimbo la Singida Magharibi, baada kujinadi kwa wananchi waliouzuia msafara wake uliokuwa ukitoka wilayani Manyoni kwenda Singida Mjini
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Jimbo la Singida Mashariki, Diana Chilolo, akipongezwa na Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli baada ya kusaidia kumnadi wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo hilo lililokuwa linaongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Chilolo alimsambaratisha Lowassa na Tundu Lissu kwamba hawastahili kuwa viongozi kwani hata katika majimbo yao hakuna maendeleo waliyoyafanya. Pia alisema afya ya Lowasa haimruhusu kuongoza nchi..
 Wananchi wa Ikungi wakishangilia wakati Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli  akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Jimbo la Singida Magharibi.
 Wananchi wakishangilia walipomzuia  Dk Magufuli katika Kijiji cha Kintinku, wilayani Manyoni.


 Wananchi wakishangilia walipomzuia  Dk Magufuli katika Kijiji cha Kintinku, wilayani Manyoni.


 Mama Mkazi wa Manyoni akishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni
 Mkazi wa Manyoni,  mkoani Singida, akishangilia huku akiwa na mwanawe baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni
 Dk. Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kutano wa kampeni mjini Manyoni, Singida leo.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkazi wa Manyoni akimshikilia mtoto ili amuone Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Manyoni.
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la ManyoniMashariki , Daniel Mtuka wakati wa mkutano wa kampeni mjini Manyoni.
 Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia CCM Mkoa wa Singida, akijitambulisha kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Manyoni..PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia CCM, Nyalandu akiwasalimia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Manyoni

 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Manyoni

 Wananchi wa Itigi jimbo jipya la Manyoni Magharibi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli

 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Itigi, Manyoni

 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Manyoni Magharibi kupitia CCM, Yahya Masale

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man akitumbuiza katika mkutano wa kampeni Ikungi Jimbo la Singida Mashariki

 Dk Magufuli (wa sita kushoto) akiwa jukwaani akiangalia wakati msanii Tunda Man akitumbuiza katika mkutano wa kampeni mjini Ikungi, Singida Mashariki

 Temba na Chege wakitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni Ikungi Jimbo la Singida Mashariki

 Kikundi cha TOT kikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Jimbo la Singida Kaskazini, Diana Chilolo akimpigia debe mgombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki kupitia CCM,Jonathan Njau na Dk Magufuli wakati wa kampeni mjini Ikungi.
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi Mgombea ubunge Jimbo la Singida Mashariki, Jonathan Njau wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ikungi leo
 Dk Magufuli akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Magharibi, Eribaliki Kingu wakati wa mkutano huo wa kampeni mjini Ikungi.
Mkazi wa Kijiji cha Puma, mkoani Singida, akishangilia alipokuwa akikimbilia kumuona Dk Magufuli aliyezuiwa barabarani na wananchi wa eneo hilo ili awahutubie.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu