Thursday, October 8, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO, UHURU ONE YAANZISHA MFUMO MPYA WA MTANDAO WA 4G LTE

Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwenye mkutano juu ya kampuni ya Tigo kuanza kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.
Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo Uhuru One, Rajab Katunda (kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu mradi huo. (katikati) ni Meneja Mradi huo wa Tigo, Kobbina Awuch.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katundu wakifuatilia mkutano huo.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katunda wakiwa katika picha ya pamoja.
Meza kuu. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uhuru One, Baraka Mtunga, Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katunda, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez na Meneja Mradi huo wa Tigo, Kobbina Awuch
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
---
KAMPUNI ya Tigo imeanzisha mfumo wa kuunganisha mtandao wa 4G LTE kwa wateja wa mtandao huo na wakazi wa Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Gutierrez alisema upanuzi wa 4G umetokana na mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya majaribio yaliyofanywa na kampuni hiyo maeneo ya Mliman Cioty na Masaki Peninsula April mwaka huu.

Alisema upatikanaji wa 4G jijini kote unaridhisha na kwamba dhamira ya tigo ni kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini na kuongoza katika utoaji wa huduma zaidi na za uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa wateja.

Gutierrez alisema mtandao wa 4G LTE unamaanisha ongezeko la kasi ya kuperuzi na kupakua habari kutoka kwenye intaneti, kupiga simu kwa njia ya skype. pia inamwezesha mteja kupata mtiririko wa video au kufanya mkutano kwa njia ya mtandao kwa ubora wa hali ya juu.

"Upanuzi huu unamaanisha wateja wa tigo waliopo katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke waishio maeneo ya Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata, Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala, Mikocheni, Msasani, Sinza sasa watapata huduma bora na upatikanaji wa intaneti ya kasi zaidi kupitia mtandao wetu,"alisema Gutierrez.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ipo mbioni kuzindua huduma ya 4G katika miji ya Arusha , Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza na Tanga mwezi ujao na hivyo kuifanya kampuni hiyo kuwa na mtandao mkubwa na wa kasi zaidi wa 4G nchini.

Wakati huohuo kampuni hiyo imeanzisha ushirikiano na kuunda mfuno wa utoaji huduma za kimtandao usiotumia muindombinu asilia ya mawasiliano ambao utaiwezesha UhuruOne kupanua upatikanaji wa teknolojia ya 4G na kwamba mfumo huo ni wa kwanza barani Afrika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mradi huo kutoka Uhuru One, Rajab Katunda alisema ''Tunaiona Afrika ikichipua kiteknolojia lakini kujumuisha uwanda mpana wa mawasiliano na dijitali kwenye uchumi wetu kutautendea uchumi wetu jambo ambalo litatuneemesha sisi wenyewe na kutuinua kimaisha".

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu