Tuesday, October 6, 2015

KIIZA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SEPTEMBER SIMBA SPORT CLUB 2015

Kocha wa Simba Dylan Kerr akimkabidhi Hamisi Kiiza Tuzo ya Mchjezaji Bora wa Simba sport Club Mwezi September 2015.
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.Mshindi wa mwezi wa September, 2015 ni Hamis Kizza ambapo amepata kura 250 kati ya kura 411 zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.Akikabidhiwa tunzo na kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr, mshambuliaji wa kimataifa Hamis Kizza alisema 

“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikiwa kuwa mchezaji wa Kwanza kabisa kuchukua tunzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2015, napenda kuwaahidi wapenzi na mashabiki wangu katika mchezo wa soka kuwa sasa hii ndio itakuwa chachu yangu ya kufanya vizuri zaidi nikiwa na klabu yangu ya Simba”.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu