Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa na Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la fedha la kimataifa wa Mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye majadiliano ya kukuzauchumi katika mkutano wa MEFMI. Aliyesimama mbele ni Bi. Arunma Oteh Makamu wa Rais na Mweka hazina.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwa katika mkutano wa kamati ya maendeleo akifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mikutano hiyo yabenki ya dunia.
Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile katika ofisi ya Tanzania nchini Peru- Lima
Wapili kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Sirvacius Likwelile akisikilizwa kwa makini na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Wilson Masilingi wa pili kutoka kushoto na Bw. Said Magonya wa kwanza kulia ambaye ni Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Bw. Bedason Shallanda wa kwanza kushoto ambaye ni Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha.
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa katika majadiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia wa kundi namba 1 Afrika Bw. Louis Rene Peter Larose anayezungumza katika mikutano ya mwaka ya Benki ya dunia na (Picha zote na Ingiahedi Mduma na Eva Valerian, Peru – Lima).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: