Thursday, October 8, 2015

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YASEMA MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KUFIKIA ASILIMIA 6.1

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya watu Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hapo pichani) juu ya Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2015 umepunguwa hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Agosti mwaka huu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Ephraim Kwesigabo leo Jijini Dar es Salaam.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii).
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei  umeshuka hadi asilimia 6.1  kwa Septemba kutoka asilimia 6.4 kwa kipindi cha Agost 2015.

Akizungumza Dar es Salaam leo  Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo alisema kushuka kwa mfumuko wa bei kunachangiwa na kushuka kwa  bidhaa za vyakula zinazotumiwa majumbani na kwenye migahawa pamoja na vinywaji baridi.

Alisema mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2015 umepungua hadi kufikia asilimia 9.6 kutoka aslimia 10.2 kwa Agost 2015

''Bidhaa za huduma kwa mwaka huu Septemba umepungua ikilinganishwa na kiasi cha bei kilichokuwepo Agost mwaka uliopita ambapo farihisi za bidhaa zimeongezeka hadi 159.4 na kutoka 149.93 Septemba 2014,' alisema.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka unapima unapima kiwango cha badiliko la kiasi cha bei za bidhaa pamoja na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

''Mfumuko wa bei ambao haujumlishi bei za vyakula na   na nishati  umebakia kuwa asilimia 22 kwa Septemba 2015 kama ilivyokuwa  Agosti 2015,''alisema

Alisema thamani ya shilingi inatafsiriwa katika matumizi ya mlaji wa bidhaa mbalimbali ambapo shilingi ya Tanzania imeonekana kununua bidhaa na huduma zilezile katika vipimo tofauti tofauti.

''Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 62 na senti 88 kwa Septemba 2015 kutoka Septemba 2010,''alisema.

Mkurugezi huyo alisema farisihi za nishati na mafta zimekuwa na mwendendo wa hali ya juu kwa kipindi chote zikilinganishwa na farihisi nyingine.

Alisema mfuko wa bei kwa kipindi cha mwezi mmoja umeongezeka kwa aslimia 0.1 ukiwa umechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula  kama vile mkaa, pamoja na huduma za saluni.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu