Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 kama unavyoendelea nchi nzima baada ya Jeshi la Polisi kuvamia kituo cha kukusanya taarifa kilichopo katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi Beach. Tukio hilo

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC Wakili Harold Sungusia akizungumza kwa masikitiko katika eneo la tukio alisema “mpaka sasa hatujui kosa kwani tumekuwa tukifuatilia chaguzi mbali mbali toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini na tumekuwa tukifuata sheria na taratibu zote zinazopaswa kama waangalizi na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupa vitambulisho vya uangalizi kwa kutambua mchango na nafasi yetu”.

Hata hivyo sakata hilo bado linaendelea kwani wafanyakazi pamoja na vifaa vyao vya kazi ikiwemo kompyuta 27 pamoja na simu zao za mkononi ambavyo vimeshikiliwa na Jeshi la polisi likiongozwa na afisa mpelelezi wa Kituo cha Polisi cha Kawe aliyefahamika kwa jina la Mgonja. Wafanyakaizi wamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: