Thursday, October 15, 2015

SHINDANO LA SERENGETI MASTA LAHITIMISHWA JIJINI MBEYA NA ARUSHA

Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Daniel Mwakasungule akionja ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa ya Bondeni, Kijenge juu jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii.
 Mkazi wa Arusha na mpenzi wa bia ya Serengeti Premium Lager Laota Elias akishiriki katika shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla kwa mkoa wa Arusha katika kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager. Mashindano hayo ya mwisho yalifanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha ambapo yaliwakutanisha washindi mbalimbali wa baa za mkoa huo waliofika kuchuana vikali ili kumpata mshindi wa jumla. Kampeni hiyo imefikia tamati jijini humo baada ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa kusaka washindi waliopewa jina la “Serengeti Masta”.
 Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa Arusha Laota Elias akionyesha fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta “Serengeti Masta” wa jumla wa mkoa huo lililofanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake watatu katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia hiyo na kuibuka “Serengeti Masta” wa mkoa wa Arusha. Shindano hilo la “Serengeti Masta” limezunguka katika baa mbalimbali za jiji la Arusha likiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.
 Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta, Faraji Mbwambo akijaribu ladha tofauti za vinywaji vya kampuni ya SBL katika baa ya Mbeya Pazuri ambapo shindano la mwisho la Serengeti Masta lilifanyika mwishoni mwa wiki.. Mshindi huyo alijinyakulia kitata cha fedha taslim Tsh. 100,000 kwenye shindano hilo la mwisho ambalo limedumu jijini humo kwa muda wa miezi miwili.
Mmoja wa washiriki wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa jiji la Mbeya akitokea Power bar ya Mbalizi Maxmilian Majaliwa Kamanga akijaribu ladha tofauti za vinywaji vya kampuni ya SBL katika baa ya Mbeya Pazuri ambapo shindano la mwisho la kumtafuta mshindi wa jumla kwa mkoa huo lilifanyika mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limezunguka katika baa mbalimbali jijini humo ambapo kwa ujumla shindano hilo limewafikia wahudumu zaidi ya 4000 Tanzania nzima katika kipindi cha miezi miwili ya kampeni na kuwafunza juu ya utoaji huduma kwa wateja.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu