Monday, October 5, 2015

SIKU YA WANAFAMILIA YA KAMPUNI YA AIRTEL TANZANIA YAFANA DAR


 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana kucheza muziki chini ya bomba la mvua wakati wa bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakifurahia michezo katika bwawa la kuogelea la Hoteli ya Kunduchi Beach Wet in Wild, katika siku ya familia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakifurahia michezo ya bembea hafla ya siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakianza mashindano ya mbio za magari madogo yaendayo kasi ‘Go Kat’ katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia hao jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi na familia zao wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao pia ni sehemu ya mambo muhimu yanayochangia mafanikio kampuni yao.
 Mmoja wa watoto wa wafanyakazi wa Airtel akimpakulia mwenzake kama
ishara ya upendo wakati wa siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na baadhi ya wa wafanyakazi wa kapuni hiyo katika maadhimisho ya siku ya wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, Patrick Foya (kushoto) akimpomgeza Hagulwa Joseph,  mtoto aliyeshinda katika shindano la kusakata dansi lililofanyika kunogesha bonanza la siku ya familia ya kampuni hiyo jijini Dar es Saalaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu