Na Mwandishi Wetu, Mwanza.

Dar es Salaam. Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula ametangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya mbunge anayemaliza muda wake, Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Nyamagana, Peter Mainya, amesema jumla ya wagombea saba walichuana kuwania nafsi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa Nyamagana.

Mainya amesema, ushindi wa Mabula umetokana na msingi uliowekwa na chama chake katika matokeo ya uchaguzi wa udiwani ambapo kati ya Kata 18 zinazounda jimbo hilo, CCM imeweza kujinyakulia Kata 14 huku Kata nne zikichukuliwa na Chadema.

“Kutokana na msingi huo, Stanslaus Mabula ameweza kupata kura 81,170. Hivyo basi, kwa mamlaka niliyopewa, namtangaza Stanslaus Mabula kuwa ndiye mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Nyamagana” alisema Peter Mainya.

Ezekiel Wenje anakuwa mbunge wa pili wa upinzani kupoteza kiti chake jijini Mwanza baada ya Highness Kiwia aliyekuwa anatetea kiti chake cha ubunge katika jimbo la Ilemela kuangushwa na Anjela Mabula katika matokeo yanayoashiria kurejea kwa utawala wa CCM katika siasa za Mwanza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: