Thursday, October 8, 2015

TAARIFA ZA TAKWIMU SASA KUWEKWA HADHARANI ILI WANANCHI WATOE MAONI YAO JUU YA MAENDELEO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu wadau wa maendeleo Endelevu leo jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dk.Rogers Dhliwayo akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird akizungumza kwenye mkutano huo.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masula ya Uchumi na Kijamii (ESRF), Oswald Mashindano (Ph.D), akizungumza katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa maendeleo Endelevu (SDG’S) ambao shabaha yake kubwa iliukuwa kuweka mifumo ya namna ya kutekeleza mpango huo leo jijini Dar es Salaam
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda akizungumza katika mkutano wadau wa maendeleo Endelevu leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akihutubia kwenye mkutano huo.
Baadhi ya viongonzi mbalimbali na wananchi waliohudhulia mkutano huo leo jijini Dar es Salaa. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa serikali imesema itakusanya takwimu na kuchapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii ili wananchi waweze kutoa maoni juu ya maendeleo ya Taifa lao.

Hayo yalisemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa maendeleo Endelevu (SDG’S) ambao shabaha yake kubwa iliukuwa kuweka mifumo ya namna ya kutekeleza mpango huo.

Alisema kuwa utoaji wa taarifa hizo ni makubaliano ya kidunia katika mpango wa utekelezaji Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDG’S)

Alisema kuwa kuwa mpango wa awali uliokuwa ukijulikanana kama Mpango wa Maendeleo wa Milenia MDG’S ulikuwa na malengo manane, huku yakiwemo mapungufu kadhaa kama vile masuala ya kiuchumi ,Ajira,tofauti ya kipato na mataifa mengine pamoja na Mazingira.

Aliendelea kufafanua kuwa Malengo Mapya 17 yaliyosainiwa hivi karibuni huko newyork Nchini Marekani na marais kutoka katika mataifa mbalimbali duniani,yamezingatia mapungufu hayo nakusema kuwa katika utekelezaji wa Mpango huo wa miaka 15 hali ya kiuchumi,Ajira,Elimu,huduma ya Umeme wa viwanda pamoja Ubora itaboreshwa zaidi.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha Profesa Aldoph Mkenda amesema serikali itachukua hatua ya kuzitafsiri taarifa na kuziweka katika Lugha ya Kingereza na Kiswahili ili kusaidia wanachi kusoma na kuelewa kwa urahisi.

Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDG’S) umemalizika hivi karibuni na sasa unatarajiwa kuanza Mpango pya wa Maendeleo Endelevu SDG’S ambao utaanza kutekelezwa January Mosi 2016 na kufikia tamati mwaka 2030.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu