Friday, October 16, 2015

TASNIA YA MTINDO NCHINI TANZANIA KUUNGANA KATIKA KUSHEREKEA AMANI NA UMOJA

Rais mstaafu wa marekani marehemu, John F kennedy alisema “usiulize nchi yako imekufanyia nini , jiulize umefanya nini kwa ajiri ya nchi yako. Mitindo kama sanaa inautashi wenye nguvu ya kuwashawishi na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa amani katika jamii yetu.

Hivyo,mbunifu mkubwa wa mavazi Afrika, Mustafa Hassanali pamoja na wabunifu wengine wenye tunzo nyingi za mavazi nchini ambao ni Kiki Zimba na Martin Kadinda wamekusanya nguvu kwa pamoja na kuhubiri juu ya umuhimu wa amani katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kwa kuwa na onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe 17 oktoba mwaka huu 2015, ambalo litakalo onyesha kazi za ubunifu zilizo fanywa na wabunifu hao watatu.

Fashion for peace hina nia ya kukuza uwezo wa nguvu ya mitindo kama shombo kinacho kuza amani na maelewano katika kipindi hiki cha uchaguzi

“niki nukuu sentensi kutoka katika wimbo wetu wa taifa “Hekima,Umoja,na Amani , hizi ni ngao zetu”inaonyaesha ni jinsi gani ilivyo muhimu kwa sisi vijana kukuza na kulinda Uhuru, Amani , na Utulivu wa nchi yetu tulio rithi kutoka kwa mababu zetu ili tuweze kuufikisha kwa wajuu zetu” alisema Mustafa Hassanali

Nchi nyingi zinajua kuhusu Haki za binaadamu,mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na vita, tunania ya kubadirisha mitazamo kwa kuchunguza na kutuza (kuziba) tamaduni kwa kupitia mitindo

“uchaguzi huu mkuu ni wa muhimu sana,sisi kama vijana wa kitanzania, nawaomba vijana wenzangu wahakikishe wanapiga kura katika uchaguzi wa mwaka tarehe 25 oktoba , nasisitiza tena juu ya umuhimu wa kukaa katika hali ya utulivu kwa kufatilia na kukubali matokeo ya uchaguzi yatakayo tangazwa na tume ya uchaguzi mkuu katika hali ya Amani” alisema Martin Kadinda.

“Utu, Amani na Upendo ni maisha bora kwa kila mtanzania” alisema kiki zimba.

Onyesho la Fashion for peace ni matokeo ya kuamini kuwa mabadiliko chanya yatakuja endapo tutahacha kufatilia yaliyo hasi na kuhamasisha yaliyo mema kwa kufanya kazi pamoja katika hali ya maelewano na kusherekea mafanikio ya nchi yetu katika hali ya Umoja.

“tungependa kuchukua nafasi hii kushukuru kampuni ya 361 degrees ambao ni waandaaji wa tukio hili, washika dau katika tasnia ya mitindo, wadhamini wetu, thinkprint, king Solomon, protea hotels, Eventlites na Darling hair Tanzania “ alimalizia Mustafa Hassanali

Tuungane mikono katika kusheherekea kwa kuudhuria onyesho la mitindo la fashion for peace ambalo litafanyika tarehe 17 oktoba mwaka huu, kuanzia saa mbili na nusu jioni na kuendelea, katika ukumbi wa King Solomon huliopo Eaters Point, Namanga. Onyesho lipo wazi kwa jamii yote na tiketi zinapatikana Eaters Point na Epidor Masaki.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu