Tuesday, October 6, 2015

TCRA YATOA ELIMU KWA MENEJIMENTI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO


 Fundi Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Kenny Chitemo (aliyenyoosha mikono) akiwaonyesha Menejimenti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo moja ya mtambo wa masafa uliwekwa katika gari la masafa wakati menejimenti hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za TCRA Jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye koti la blue ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (wapili kulia) akiangalia mtambo wa masafa uliokua ukionyeshwa na Mhandisi Mwandamizi Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw.Robson Shaaban (kulia) wakati Menejimenti ya Wizara hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za TCRA Jijini Dar es Salaam.
Menejiment ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikimsikiliza kwa makini Mhandisi Masafa kutoka TCRA Bi. Imelda Salum (kushoto) wakati Menejimenti hiyo ilipofanya ziara katika ofisi ya TCRA Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Uongozi kutoka TCRA wakati wa ziara iliyofanywa na Menejimenti ya Wizara ya Habari katika ofisi za TCRA kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Zamaradi Kawawa akifafanua jambo wakati wa ziara iliyofanywa na Menejimenti ya Wizara Habari kujifunza mambo mbalimbali katika ofisi ya  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu