Mbunge viti maalumu kupitia Wazazi Phide Mwakitalima ambaye naye aliongozana na vijana hao katika kuhamasisha kumchagua kiongozi anaefaa kuongoza jiji la Arusha na kuleta maendeleo

 
Mbunge wa viti maalumu Phide mwakitalima akiwa anamuamasisha mmoja wa mfanyabishara kuchagua kiongozi anaefaa siku ya Oktoba 25, 2015.
 baadhi ya vijana hao wakiwa wanaonyesha hisia zao
 pia kulikuwa na mechi walioiyandaa  yote haya yalikuwa ni kuamasisha kumchua kiongozi ambaye anaeweza kuibadilisha mkoa wa Arusha pamoja na kata zake
 hapa baadhi ya vijana waliamua kupiga push shap huku wakisema hapa kazi tu.

Habari picha na woinde shizza,Arusha
 
Wananchi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake wametakiwa kukataa mihemko ya kampeni za uchaguzi ili isiwe chanzo cha kuwagawa na kuwagombanisha wao kwa wao kwani kuna maisha baada ya uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya vijana kutoka katika vyama mbalimbali vya siasa mkoani  Arusha wakati walipokutana kuzungumzia hatma ya jimbo lao la Arusha mjini.

walisema kuwa kwa mkoa wa arusha kumekuwa na mhemko ya siasa ambayo imewatawala sana vijana hali ambayo inapelekea uvunjifu wa amani na hata kuleta ugomvi.

Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Sauli Melayeki ambaye alitokea katika kata ya Olasiti alisema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi  kuachana na miemkoa ya kisiasa na kutambua kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.

Alisema kuwa imefikia wakati vijana kukaa chini na kutafakari na kufanya siasa zamsingi na kuacha siasa za ushabiki ambapo zinapekea kuchagua kiongozi mradi kiongozi bila hata ya kumuangalia kama ana faa au hafai.

Alisema kuwa kwa kipindi hichi wananchi wa jiji la arusha wanatakiwa wakae chini wafanye tasimini wawaangalie viongozi wote kutoka vyama vyote ambaowanagombania nafasi mbalimbali za uongoz i wakianzia wabunge pamoja na madiwani wao waaangalie uelewa wao au kama watafakuwaongoza na kuweza kukuwawakilisha vyema wananachi wao katika sehemu husika na sio wale viongozi ambao watakuwa wanasababisha uvunjifu wa amani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: