Na John Gagarini, Chalinze.
Mwanasiasa mkongwe nchini na mwenyekiti wa chama cha Democratic Party mchungaji Christopher mtikila (62)  amefariki dunia jana baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea oktoba 4 majira ya saa 11:45 alfajiri huko chalinze kijiji cha msolwa kata ya bwiringu wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani barabara ya kuu ya Dar es salaam-Morogoro.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Jafary Ibrahim alisema kuwa katika tukio hilo  watu wengine watatu walijeruhiwa.
"Marehemu na wenzake walikuwa wakitokea mkoani Njombe kuelekea jijini Dar es salaam wakitumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili t 189 AGM  ambapo alisema liliserereka umbali wa kama mita 150 hadi 200 na kupasuka kioo cha mbele na kusababisha kifo chake," alisema Ibrahim.
Kamanda Ibrahim alisema kuwa watu waliojeruhiwa ni dereva wa gari hilo George Steven (31) maarufu kama ponera mkazi wa mbezi, Patrick Mgaya (57) Ally Mohammed (42) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam ambao wamelazwa kwenye hospitali ya tumbi.
Aidha alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi ambapo gari hilo liliharibika kwa kioo cha mbele na nyuma kutoka pamoja na matairi kupasuka.
Baadhi ya watu walisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea abiria hao walikosa msaada kwani eneo hilo halina makazi ya watu.
Wakati huo huo wananchi wengi wameelezea masikitiko yao kwa vitendo vya watu wengi kurusha picha ya mwili wa marehemu Mchungaji Mtikila ukiwa umelazwa pembeni ya kinachoonesha ni gari alilokuwa akisafiria kabla ya kupata ajali.
 
Pichani ni mabaki ya gari alilokuwa akisafiria Marehmu Mchungaji Mtikilia na abiria wengine watatu.
Wengi waliowasiliana na ofisi zetu wameitaka TCRA kuwa wakli na sheria zilizopo na ambazo tayari zimeshaanza kutumika zitumike na zioneshe zinatumika".
Kwa kweli inatia uchungu sana kuona badi ya Watanzania sijui kwa ujuaji sana ama kwa kutaka sifa kwenye magurupu huko wamerusha picha ya mwili wa Mch. Mtikila.
"Nimeiona na sikupendezwa nayo kabisa", amesema Benjamin Mbozila akiwa jijini Nairobi. "Afadhali wangerusha ile ya gari tu, lakini mwili mzima na sura inaonekana sio sawa kabis", Janeth Mtonyi alieko ujerumani ametuandikia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: