Wasimamizi wa Uchaguzi nchini wametakiwa kusimamia sheria katika kutekeleza majukumu ya kusimamia Uchaguzi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Mwenyekiti wa Uchaguzi Jaji mstaafu Damiani Lubuva amesema hayo katika hotuba ya ufunguzi kwa Wasimamizi wa Uchaguzi toka majimbo yote nchini kwa lengo la kupata uzoefu kuboresha utendaji kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Mpaka sasa zoezi la kampeni linakwenda vizuri tufanye kazi zetu kwa weledi, kila mmoja wetu ashiriki kikamilifu katika mkutano huu, ili kuweza kupata michango itakayoweza kufanikisha uchaguzi huru, haki na amani ukizingatia kwamba wengi wenu ni wazoefu, kupitia wakati huu mtaweza kushirikishana uzoefu na kujifunza”

Aidha Lubuva ameongeza kuwa NEC imehusisha jeshi la polisi kwa lengo la kupata maoni yao ya namna ya kusimamia Uchaguzi na kuwataka washiriki wote kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha amani inakuwako na itaendelaa kuwako hata baada ya `uchaguzi.

Wakurugenzi hao wametakiwa kutomruhusu mtu au kikundi cha watu, vijana kusimama karibu na vituo vya kupigia kura kwa madai ya kulinda kura hii ni kukiuka taratibu na sheria na kuwasihi wawe na ushirikiano na kuwa karibu na NEC wakati wote wa shughuli za Uchaguzi kwa lengo la kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani
Maofisa wa NEC wakifuatilia kwa makini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Ernest Mangu, akifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wasimamizi wa Uchaguzi toka majimbo yote nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi nae amehudhuria.
Maofisa wa Jeshi la Polisi nao wakifuatilia kwa makini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: