Mkuu wa Huduma za Kifedha Kwa Njia ya Mtandao wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Wateja wa Tigo Pesa kupata faida ya robo mwaka ya shilingi bilioni 3.8. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.
---
Na Mwandishi Wetu.

KAMPUNI ya Tigo Tanzania imefanya malipo mengine ya gawio la faida ya kila robo mwaka kwa wateja wake kiasi cha shilingi za ki-tanzania bilioni 3.884. Hili ni gawio la pili la robo mwaka kwa mwaka huu na ni zaidi ya asilimia 17 ya bilioni 3.3 ambayo ililipwa na kampuni katika robo ya pili.

“Lengo letu ni kuhakikisha wadau wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa biashara kugawana faida hii kulingana na kiasi kilichohifadhiwa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa," alisema hayo mkuu wa huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel

Haya ni malipo ya sita katika robo mbalimbali za mwaka ambazo Tigo imekuwa ikitoa kama faida iliyozalishwa kutoka kwenye akaunti ya Tigo Pesa ijulikanayo kama Trust inayofanywa na benki kubwa nchini Tanzania. 

“Tumefurahi kwa mara nyingine tena, kwa kutangaza gawio hili kwa wateja wetu waaminifu wa Tigo Pesa. Malipo haya yanadhihirisha dhamira yetu ya kutoa huduma za kifedha kwa wateja wetu na nchini kwa ujumla,” alisema Swanepoel.

Mwezi Julai, 2014 kampuni ya Tigo ilikuwa ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano ya simu duniani kutoa gawio la faida yake katika akaunti ya Trust, katika mfumo wa ugawaji wa kila robo mwaka kwa watumiaji wake wa Tigo Pesa.

Akifafanua kuhusu malipo, Swanepoel alisema kuwa kabla ya rejesho  kwa wateja, hufanyiwa ukokotoaji kulingana na wastani wa salio la kila siku lililotunzwa kwenye akaunti zao za Tigo Pesa. Alitoa mfano wa sababu ya ongezeko la malipo,kuwayanatokana na ongezeko la jumla  ya masalio katika akaunti ya Trust na wateja zaidi na zaidi kujiunga pamoja naongezeko la utumiaji waTigo Pesa kwa wateja waliopo.

Mpango wa utoaji wa faida ni kwa mujibu wa agizo la benki kuu lililotolewa mwezi Februari mwaka 2014. Hadi sasa kampuni imelipa jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 31.1 tangu kuzinduliwa kwa mpango huu mwaka uliopita, kwa mujibu wa Swanepoel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: