Wednesday, October 7, 2015

ZIJUE FAIDA ZA KUWA NA CHETI ZA KUZALIWA

Kumiliki cheti cha kuzaliwa Tanzania ni jambo muhimu; Mtoto anapata haki za msingi na kufurahia matunda ya nchi yake iwapo atakuwa ametambulika kihalali katika nchi aliyozaliwa. 

Ndani ya mwaka 2013, mfuko wa kimataifa wa watoto (UNICEF) ilitoa takwimu ya zaidi ya watoto millioni 230 katika nchi zinazoendelea hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa. (Ripoti ya utafiti Canada, 2014).

Tanzania ikiwa moja kati ya nchi za mwisho kati ya Afrika mashariki na kati yenye kiwango cha chini cha uandikishaji kwa watoto chini ya miaka mitano, iliweza kujikwamua kwa kuongeza idadi kubwa ya uandikishaji kupitia njia mpya ya simu ya mkononi iliyoanzishwa na RITA, mwaka 2013
Hata hivyo, zaidi ya 80% ya watoto wa vijijini wa chini ya umri wa miaka 5 Tanzania bado hawana vyeti vya kuzaliwa. 

Wazazi wamekuwa wakijifungua majumbani na kushindwa kufuatilia jinsi ya kufanya uandikishaji kutokana na umaskini, umbali wa vituo, na uelewa mdogo wa faida zake.

“Tangu wazazi wangu walipofariki nilipokuwa mdogo sikuweza kupata cheti changu cha kuzaliwa na hakukuwa na mtu muhimu wa kufatilia, hivi sasa nahitaji kusoma, kupiga kura, kadi ya utambulisho wa taifa na misaada mingi ya kunikwamua kimaisha lakini nilikosa huduma hizo mwanzo, hivyo nimekua mkubwa wa kujitegemea na nitafanya jitahada nipate haki yangu ya msingi”, alizungumza binti Innocensia Leizer (18).

“Nilipoteza cheti changu cha kuzaliwa na nilishindwa kupata hati ya kusafiria, nashukuru sasa nimefanya ufatiliaji na nimeipata hati yangu, nitasafiri kwenda India kimasomo”. (mkazi wa Dar es Salaam).

Andrea Guzzoni, Meneja mkazi wa JovagoTanzania alifafanua kuwa “Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu inayothibitisha umri wa mototo na mahali alipozaliwa, hivyo inamsaidia pia kumlinda kisheria iwapo itatokea sababu yoyote itakayo hitaji kuthibitisha vitu hivyo vya msingi kimahakama”

Vyeti hivi pia vinafaida katika Elimu; Mtoto hawezi kupata elimu ya aina yeyote kuanzia ngazi ya msingi mpaka chuo kikuu kama hatokuwa na cheti chamkuzaliwa.

Pia ni muhimu katika kutafutia hati za kusafiria (Passport); Hakuna sheria inayoruhusu mtu kupata passport kama hakuwa na cheti cha kuzaliwa, hii inasaidia kutambua kama muombaji anatambulika na serikali ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

Afya; cheti hiki pia ni muhimu kwenye masuala ya afya, baadhi ya huduma za kiafya hazipatikani bila ya cheti cha kuzaliwa.

Vitambulisho vya utaifa na vya kupigia kura; vitambulisho hivi ni muhimu kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi, hauwezi kupata kadi yako ya utambulisho wa taifa pasipo na cheti cha kuzaliwa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu