Saturday, November 14, 2015

DEOGRATIUS NGALAWA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA LUDEWA

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyofanyika leo tarehe 12 Novemba, 2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete imemteua Ndugu Deogratius Ngalawa kuwa mgombea wake wa Ubunge katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.

Ndugu Ngalawa ameteuliwa kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kushinda kura za maoni zilizofanyika Novemba 10, 2015.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu