Thursday, November 26, 2015

HALI YA ZANZIBAR NI SHWALI KABISA NA SHUGHULI ZA KUJENGA TAIFA ZINAENDELEA

Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar ameyataka mataifa kuacha kupotosha ukweli wa hali ya usalama wa Zanzibar na vitongoji vyake.

Akizungumza katika Mahojiano maalum baada ya Kajunason Blog kutembelea ofisini kwake kutaka kujua mustakabali wa hali ilivyo ambapo alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakiongea uongo jambo ambalo si sawa na kuwa hali ya Zanzibar wananchi wametulia na wananendelea na shughuli zao za kila siku.

Aliongeza kuwa hakuna machafuko yeyote yale, watu wanaendelea kuchapa kazi wakisubiri siku itakayotangazwa uchaguzi na wao waanze kufanya kazi.

Kajunason Blog iliingia mitaa kadhaa ya mji wa Zanzibar na kujionea wananchi wakiendelea kuchapa kazi kama kawaida jambo ambalo limeoneka ni jema tofauti na watu wengi wanavyoizungumzia.

Akiongea Bwana Juma Ally ambae ni Mkazi wa Zanzibar alisema wanamshukuru Mungu kwa kila linaloendelea na wao wapo tayari kurudia uchaguzi pindi utakapopangwa na Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). 

Wananchi wakiwa eneo la Darajani wakiendelea na shughuli zao za kujenge taifa.
Mtangazaji wa RFI- Kiswahili, Victor Abuso akifanya mahojiano na wananchi wa mji wa Zanzibar wakielezea machache juu ya hali ya usalama.
Biashara ya Samaki ikiendelea.
Maskani ya vijana wa CUF na CCM wakiwa pamoja!
Hawa ni Wazee na Vijana wa Zanzibar wakiomba dua ili mwenyezi Mungu aendelee kuuweka mji wao salama.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu