Friday, November 13, 2015

HATUA YA PILI YA KWENDA KUWA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - PETER SARUNGI

Ndugu, jamaa na marafiki, napenda kusema shukrani zangu kwa wale wote walionitia moyo na kunishauri juu ya nia na safari yangu ya kuwa spika wa bunge. Asanteni sana na mungu azidi kuwabariki.

Sasa niombe jambo la pili katika hatua ya kwenda kuwa spika. Mpaka sasa naendelea na mikakati ya kuniwezesha kufanya kampeni vizuri na kwa ushindani mkubwa nitakapofika dodoma, Lakini ni ukweli usiopingika kuwa kuna gharama za kufanya kampeni. Nimejianga kufanya kampeni nikiwa na kamati ndogo lakini yenye ushawishi mkubwa. Kamati yangu itakiwa na watu 12 pamoja na mimi tutakoweka kambi kwa siku 5 tukifanya kampeni. Hivyo niwaombe kwa unyenyekevu mkubwa ushiriki wako katika kutimiza ndoto za watu wenye ulemavu kwa kuchangia chochote ulichonacho na kwa kadri utakavyogusa kwenye kujenga historia hii. Kampeni zangu zitagharimu Million 6 tu na michango yako itapokelewa kupitia namba zifuatazo:

+255713037798 au +768426868 zote zikiwa zimesajiliwa kwa jina la Peter sarungi.

Tafadhali shiriki katika kutengeneza historia ya watu wenye ulemavu kwenye ushiriki wa vyombo vya maamuzi. Kutoa ni moyo na wala si utajiri. Tafadhali Like, Comment, Share na Changia ili ujumbe huu ufike kwa watanzania wote wanaojali na kuguswa na makundi maalum ikiwemo ya watu wenye ulemavu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu