Saturday, November 7, 2015

JE WAJUA MAAJABU YA AUGUSTINO LYATONGA MREMA?

(1) AGUSTINE LYATONGA MREMA  ndiye mbunge pekee aliyewahi kuwa mbunge katika majimbo matatu tofauti hapa Tanzania? 
1. MOSHI VIJIJINI 2. TEMEKE 3. VUNJO.

(2) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye Mtanzania pekee aliyewahi kuwa mbunge kupitia vyama vitatu tofauti? 
1.1980 - 1995 MOSHI VIJIJINI (CCM), 2. 1996 - 1998 TEMEKE (NCCR- MAGEUZI), 3. 2010 - 2015 VUNJO (TLP).

(3) AGUSTINE LYATONGA MREMA amewahi kuwa mwanachama wa vyama vitatu vya siasa nchini 1. CCM (1977 - 1995), 2. NCCR - MAGEUZI (1995 - 2000), 3. TLP (2000 - 2015).

(4) Majimbo yote ambayo AGUSTINE LYATONGA MREMA amewahi kuwa mbunge yameongozwa na vyama vitatu tofauti tu, 
1. MOSHI VIJIJINI (CCM, NCCR - MAGEUZI na CHADEMA), 2. TEMEKE (CCM, NCCR - MAGEUZI, na CUF), 3. VUNJO (NCCR - MAGEUZI, TLP na CCM).

5. AGUSTINE LYATONGA MREMA amegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA mara TATU (3). 1995, 2000 na 2005.

(6) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye mtanzania pekee aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, cheo ambacho hakitambuliki kikatiba wala kisheria Tanzania wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani.

(7) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye mwanzilishi wa polisi jamii (SUNGU SUNGU) Tanzania.

8) AUGUSTINE LYATONGA MREMA, Ndiye mwanasiasa pekee alieweza mnadi Raisi wa chama tofauti na chama chake huku chama chake kikiwa kina mgombea wa nafasi ya Uraisi (Alimnadi Kikwete 2010 na Pia alimnadi Magufuli 2015.

Je, kipi ambacho bado hajafanya?.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu