Friday, November 13, 2015

JUMUIYA YA ULAYA (EU) YAUPATIA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA RUZUKU YA EURO 200,000 KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MAENDELEO HAPA NCHINI


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) wakisaini hati ya mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000 kwa ajili ya Maendeleo Zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania. (Picha Geofrey Adroph wa pamoja blog)


Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ruzuku kwa ajili ya Shughuli za mendeleo hapa nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.


Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakirekodi tukio hilo.

Pichani juu na chini baadhi ya wanahabari, wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya pamoja na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (katikati) baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Picha ya pamoja na mabango yenye malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Na Mwandishi wetu.

---
JUMUIYA ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN),ikiwa ni ruzuku ya Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478,000,000 fedh a taslimu za kitanzania kwa ajili ya kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania.

Utilianaji saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro Rodriguez na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Filiberto Sebregondi.Aidha utiaji wa saini hizo ulifanyika katika Ofisi za EU jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ulaya.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.

Aidha alisema ruzuku hii imetolewa kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa imelenga kusaidia miradi ya pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) pamoja na Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano katika program kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile IOM, UNICEF, UNDP, UNODC, UNHCR, FAO, UNESCO, IFAD, UN Women na WFP.

Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa kutiliana saini alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU na UN ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.

Rodriguez, alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambapo amesema “Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu