Tuesday, November 17, 2015

THE AFRICA ENTERPRISE CHALLENGE FUND (AECF), YAZINDUA MRADI WA SHINDANO LA KUHAMASISHA MAWAZO YA KILIMO JIJINI DAR

Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya International Tan Feeds Ltd, Bw. Faustine Lekule, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, juu ya uzinduzi wa mradi wa shindano la kuhamasisha mawazo ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili ya Tanzania (TZAW R4). Pembeni yake ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa The Africa Enterprise Challenge Fund” (AECF), Sam Ng’ang’a,
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo. (Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii).
---
“The Africa Enterprise Challenge Fund” (AECF) ilizindua awamu yake ya nne ya dirisha la ufadhili wa kilimo cha biashara maalum kwa ajili ya Tanzania (TZAW R4). TZAW R4 ni shindano lenye lengo la kuhamasisha mawazo ya kilimo biashara kwa kufadhili waombaji watakaofanikiwa kwa kuwapatia ruzuku na mikopo isiyo na riba kati ya dola za Kimarekani laki moja (100,000) na milioni moja (1,000,000). Kipindi cha maombi ni kuanzia tarehe 17 Novemba hadi tarehe 15 Disemba 2015.

Shindano hili liko chini ya usimamizi wa KPMG and linapata ufadhili wa kiasi cha dola za kimarekani milioni nane (takribani shilingi bilioni 17 za kitanzania) na serikali ya Uingereza (UKAid) kupitia Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID), likiwa na lengo la kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi kwenye kilimo biashara na huduma za kifedha vijijini na kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa soko hapa Tanzania. Shindano hili linatafuta mawazo mazuri ambayo yatasababisha kukua kwa uchumi vijijini hapa Tanzania.

Shindano hili liko wazi kwa makampuni ya ndani na ya kigeni yenye lengo la kufanya kazi Tanzania, na yanayotaka kuimarisha sekta ya kilimo kwenye maeneo makuu mawili: kwanza, kwenye kilimo cha biashara katika mnyororo wa thamani wa shughuli zote zinazohusu kilimo; pili, ni kupata ufumbuzi utakaoongeza huduma za kifedha vijijini na taarifa katika kusaidia uzalishaji katika kilimo cha kibiashara na sekta zinazohusiana. Ili kufuzu mawazo ya biashara lazima yaonyeshe matokeo chanya kwa watu maskini vijijini nchini Tanzania, kutoa ongezeko la ajira na mapato, kupunguza gharama na kuongeza uzalishaji.

"Natazamia kuona ushiriki mpana wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Tanzania katika shindano hili," alisema Mkurugenzi wa AECF, Hugh Scott. Aliendelea kwa kuipa changamoto sekta binafsi "kuchangamkia fursa iliyotolewa na mfuko wa AECF TZAW R4 na kuitikia kwa kuwa na mawazo ya biashara yenye ubunifu ambayo yataleta manufaa kwa maisha ya Watanzania waishio vijijini."

Kupitia mashindano ya TZAW, na kama ilivyokuwa kwa awamu zilizopita, AECF inalenga kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi katika uzalishaji wa kilimo cha biashara na ufadhili vijijini na kuleta mabadiliko katika mfumo wa soko nchini Tanzania, na hasa Afrika Mashariki kwa ujumla. TZAW inatafuta mawazo yaliyo bora zaidi ya biashara ambayo yatasababisha ukuaji wa uchumi vijijini nchini Tanzania.

Hapa Tanzania hili ni shindano la nne kufanyika.Awamu ya kwanza ilizinduliwa Novemba 2011 na kampuni 10 zilipata ufadhili; awamu ya pili ilizinduliwa Juni 2012 na kampuni 10 zilipata ufadhili na awamu ya tatu ilizinduliwa Januari 2014 na kampuni 17 ziliidhinishwa kupata ufadhili.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu