Tuesday, November 3, 2015

NAIBU KATIBU MKUU MPYA MAMBO YA NDANI AANZA KAZI RASMI

Pix 1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE, Obedi Mbaga.
Pix 2
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akijitambulisha mbele ya Naibu Katibu Mkuu mpya, John Mngodo (hayupo pichani) wakati wa Mkutano kati ya Watumishi na Naibu Katibu Mkuu huyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara.
Pix 3
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.
Pix 4
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara (hayupo pichani) alipofanya mkutano na watumishi hao mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu