Monday, November 16, 2015

NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIFIKISHA NILIPO - KASSIM MGANGA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Kassim Mganga, amedai kwamba alipokuwa kwenye kundi la Tip Top Connection alikuwa kama mtoto wa kambo kutokana na kutokushirikishwa kwenye mambo mbalimbali ya kundi hilo.

Akihojiwa katika kipindi cha Mkasi, alisema alipokuwa kwenye kundi hilo alikuwa akiwekwa kando na hakujua sababu ilikuwa nini.

“Babu Talle hakuwa baba bora kwangu, naweza kusema hivyo kwani alinifanya nijisikie kama mtoto wa kambo, hakuwa akinishirikisha chochote,” alisema.

Alisema kutokana na kutokuridhishwa na hali hiyo, aliamua kujitoa na kuamua kufanya kazi zake mwenyewe ambapo kwa sasa anajivunia kwa kazi zake kukubalika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu