Saturday, November 7, 2015

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA KAZI KWA KUMWAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, IKULU DAR

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimina na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati aliwapowasili kwenye Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam,leo asubuhi Okt. 6, 2015 kwa ajili ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, aliyemteua jana Okt 5, 2015 mara tu baada ya kuapishwa rasmi. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Okt. 6, 2015.
 Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki na watumishi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiwa na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, baada ya kuapishwa leo wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,(kushoto) akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (katikati  wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu