Friday, November 27, 2015

RAIS DKT. MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO (TRA)

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.

Rais Magufuli pia amemteua Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.

Taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu