Monday, November 23, 2015

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MADEREVA TANZANIA (TADWU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anamtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU) kufuatia kifo cha aliyekua Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Rashid Salehe kilichotokea Tarehe 20 Novemba, 2015 katika Hospitali ya Taifa Mhimbili.
Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu shupavu, mkweli, makini na aliyependa kupigania haki pale alipoamini kuwa panastahili haki hiyo na alithibitisha kwa kupigania uanzishwaji wa Chama Cha Madereva na kusimama kidete kutetea haki zao.

"Nawatakia moyo wa uvumilivu familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki,  madereva na wengine wote ambao wameguswa na kifo cha Rashid Salehe na wote tuungane kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi".

Dr Magufuli anaungana na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu na kwamba taifa litauenzi mchango mkubwa alioutoa marehemu Rashid Salehe.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu