Thursday, November 12, 2015

SERIKALI: MADUKA YA DAWA YALIYOPO PEMBEZONI NA HOSPITALI KUONDOLEWA NCHINI

pic+katibu+afya
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando.

Na Rabbi Hume

Serikali nchini, kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipo mbioni kufanya mazungumzo na wamiliki wa maduka ya madawa yaliyopo pembezoni na hospitali za serikali ili kuona uwezekano wa kuhamisha maduka hayo kutoka maeneo ya hospitali ilikuondoa utata uliopo sasa wa baadhi ya watendaji na wafanyakazi wa hospitali hizo kutumia mwaya huo wa kuhamisha madawa na kuweka kwenye maduka hayo.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mbando wakati akizungumza na waandishi mapema leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ziara aliyofanya katika baadhi ya hospitali zilizopo hapa nchini ikiwemo jiji la Dar Es Salaam na kuweka wazi mipango hiyo ya Serikali ya kuhamisha maduka hayo.

Mbando amesema kuwa kuamishwa kwa maduka hayo kutasaidia kupunguza ukosefu wa madawa katika hospitali za serikali ambapo kumekuwa kukihisiwa kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wa hospitali wamekuwa wakizuia upatikanaji wa dawa hospitalini ili wagonjwa waende kununua dawa hizo katika maduka yao yaliyo nje ya hospitali.

“Tayari tumepanga mkakati ili tuweze kuzungumza na wamiliki wa maduka ya madawa ili waweze kuhamisha maduka hayo kutoka maeneo ya hospitali za serikali na hilo agizo lazima litimizwe maana hata usajiri wa maduka yao upo kiserikali,” amesema Mbando.

Aidha pamoja na mkakati huo wa kuamisha maduka hayo pia Katibu mkuu huyo ameyagiza hospitali zote nchini kufungua maduka ndani ya hospitali ambayo yatawawezesha wagonjwa kununua dawa hapo hapo hospitali na kuipongeza hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa kufungua maduka matatu na moja likitoa huduma masaa 24.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu