Monday, November 9, 2015

TIGO YAOMBA WATEJA WAKE RADHI KWA KUKATIKA KWA HUDUMA ZAKE

Kampuni ya simu ya Tigo imeomba radhi wateja wake kutokana na kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana.

Taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imesema kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu zilizo nje ya uwezo kwa kampuni zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu tofauti tofauti.” Aidha taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba “tatizo hilo sasa limeshughulikiwa kikamilifu na huduma zote za Tigo zimerejea katika hali yake ya kawaida.’’

“Tuna sikitishwa na usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika kwa huduma zetu natunapenda kuwahakikishia wateja wetu dhamira ya kampuni yetu kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa hali ya juu, za kutegemewa na kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.

Aidha Gutierrez ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa uvumilivu wao na kutangaza kwamba kama ishara ya kuomba msamaha kampuni ina wapa wateja wake wote dakika 10 za muda wa maongezi, SMS za bure kwenda mtandao yote na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo. Kifurushi hiki mteja ana kipata kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu