Sunday, November 15, 2015

WATANZANIA WENGI HAWAWEKI AKIBA; MOSHINGI

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba, Kenya, Bi.Anne Karanja, (Katikati), na Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Posta Uganda, Bw. Stephene Mukweli, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wan ne wa Bodi ya Wadhamini, ya Umoja wa Mabenki ya Afrika Mashariki, ASBEA, uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Habari picha na K-Vis Media/Khalfan Said)

AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, amewahimiza wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye akaunti zao.

Bw. Moshingi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kutano wanne wa bodi ya wadhamini §ya Umoja wa Mabenki ya Akiba wa Nchi za Afrika Mashariki, (ASBEA), uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

“Lengo la Umoja huu ni kuhamasishawananchi wan chi wanachama wa ASBEA, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kama njia ya msingi ya kutokomeza umasikini, kimarisha uchumi na kujenga uwekezaji wenye faida katika uchumi wa mataifa yetu.” Alisema

Afisa Mtendaji huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya, (KPOSB), Anne Karanja, na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta nchini Uganda, Stephene Mukweli, pamoja na wajumbe wengine, alisema Nchi za Afrika Mashariki bado zipo nyuma kwenye suala zima la uwekaji akiba na kutolea mfano Tanzania, ambapo alibainisha

“Takriban asilimia 14 tu ya wananchi wa Tanzania ndiowanaojiwekea akiba kwenye akaunti zao, kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na asilimia 23 ambayo ndio wastani wa nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara.” Alisema Bw. Moshingi.

Umoja huo wa ASBEA ulioanzanishwa mnamo mwaka 2001, unakusudia kupanua wigo wa wanachama wake ambapo uko kwenye majadiliano ili kuzishawishi nchi za Rwanda, Burundi na Sudani Kusini kujiunga na umoja huo.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya,Anne Karanja alisemaukuaji wa teknolojia umeleta changamoto kubwa katika sekta ya kibenki barani Afrika na hivyo ni wajibu wa       wa ASBEA kuangalia namna bora ya kuitumia
teknolojia hiyo katika kuzipeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi
ili kukuza uchumi wao na nchi wanachama kwa ujumla.

Jumuiya ya ASBEA inajumla ya wateja milioni 3, wanaoweka takriban akiba ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 314 katika amana, wakijivunia utoaji huduma kupitia
mawakala, magari ya kutolea huduma, matawi ya Benki na ATMs.
 Wajumbe wakimsikiliza mtoa mada, Mkurugeni Mtendaji wa Benki ya Posta Kenya, Bi.Anne Karanja
 Bi. Anne Karanja
 Bw. Stephene Mukweli
 Bw. Sabasaba Moshingi
 Mjumbe akizungumza
 Wajumbe wakisikiliza kwa makini
 Mjumbe kutoka Tanzania kifuatilia kwa umakini mkutano huo
 Afisa wa Benki ya Posta Tanzania, akifuatilia mad zilizokuwa zikitolewa


 Wajumbe wa bodi ya ASBEA, wakiongozwa na Bw. Moshingi, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mkutano wao na malengo yake

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu