HATIMAYE Rais Dk. Johm Magufuli amemteua mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa Kassim kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.

Rais Magufuli alikabidhi jina la mteule hiyo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye naye alilitangaza kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara baada ya Spika Ndugai kutangaza jina hilo kwa wabunge, bunge lilipuka mayowe ya kushangilia uteuzi huo.

Kwa mujibu wa kanuni za bunge, baada ya jina hilo kutangazwa, wabunge walilazimika kupiga kura kwa ajili ya kuidhinisha uteuzi huo.

Idadi kamili ya wabunge wanaotakiwa kuwepo bungeni ni 394, waliosajiliwa ni 369, lakini waliopiga kura ya kuthibitisha jina hilo walikuwa 351.

Akitangaza matokeo ya kura hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema kura zilizoharibika zilikuwa mbili, sawa na asilimia 0.06, zilizosema hapana zilikuwa 91, sawa na asilimia 25 na zilizosema ndio zilikuwa 258, sawa na asilimia 73.5.

Kutokana na matokeo hayo na kwa mujibu wa kanuni za bunge, Spika Ndugai alimtangaza rasmi Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya wa serikali ya awamu ya tano.

Hafla ya kumuapisha Majaliwa inatarajiwa kufanyika jioni leo kwenye viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.
---
WASIFU WA MHE. KASSIM MAJALIWA.
Jina la Ukoo: Majaliwa
Jina la Kwanza: Kassim
Jina la Kati: Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa: 1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa: Nimeoa
Kundi: Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia: M
Simu ya Ofisi: -
Simu ya mkononi: 785205910
Barua pepe: majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani:

P.O.Box 51,
Ruangwa

Elimu
Toka Hadi Jina la Shule/Chuo Cheti

1970 1976 Mnacho Primary School cheti cha Elimu ya Msingi
1977 1980 Kigonsera Secondary School CSEE
1991 1993 Mtwara Teachers College -
1994 1998 University of Dar es Salaam Bachelor Degree
1999 1999 Storckolm University PGDP

Mafunzo Mengineyo

Uzoefu
Toka Hadi Jina la Mwajiri Ngazi/Wazifa
2015 2020 - MB
2010 2014 - MB
2006 2010 PM Mkuu wa Wilaya
2001 2006 PS-CWJ Katibu Mkoa
2001 2001 PS-CWJ Katibu Wilaya
1988 2000 PS-Moec Mkufunzi
1984 1986 TD-Lindi Council Mwalimu

Burudani
Soccer
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: