Friday, December 18, 2015

MHAGAMA; alitaka SHIVYAWATA kuondoa tofauti zao

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), (katikati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Amon Mpanju wakati shirikisho hilo lilipo kutana na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (wa kwanza kushoto), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam, (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bibi. Regina Kikuli.
Mkalimani wa lugha ya alama akifafanua mazungumzo kwa alama kwa baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakati wa mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (hayupo pichani), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakifuatilia mazungumzo ya mkutano huo, wakati wa mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mara baada ya kukutana na wajumbe wa shirikisho hilo jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
---
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), amelitaka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuondoa tofauti zao ili kuweza kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuimarisha na kulinda haki za watu wenye ulemavu.

“Mnapaswa kuhakikisha kuwa wale wote wanaoleta tofauti zenu kuwashughulikieni mapema katika vikao vyenu ili muweze kushirikiana na sisi katika kuhakikisha mnapata haki ya kulindwa , kuheshimiwa na usalama. Tunataka nchi yetu baada ya miaka mitano iwe katika historia nzuri kwa kuwajali watu wenye ulemavu”. Amesema

Ametoa wito huo wakati akizungumza na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.

Bibi Mhagama alisema: “Tunapaswa tusimuangushe Rais Magufuli kwa imani aliyoionesha kwenu na kuteua Naibu waziri anayeshughulikia masuala yanayowahusu ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,” alisema.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Amon Mpanju pamoja na kumshukuru Waziri na Naibu Waziri anayeshughulikia (Watu wenye ulemavu) kwa kuitisha mkutano uliolenga kujadili vipaumbele vya watu wenye ulemavu nchini pamoja na nchi zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi alimuomba waziri huyo kuhairisha ili waweze kukamilisha uaiinishaji changamoto zao vizuri.

“Tunaomba mheshimiwa waziri utupatie muda zaidi tuweze ili tuweze kuainisha vizuri zaidi changamoto zetu ambazo naamini Naibu waziri mwenye dhamana ya kushughulikia watu wenye ulemavu amabye pia tunaimani naye sana ataweza kubaini masuala yanayotuhusu na kuweza kuyatekeleza katika majukumu yake” alisema.

Mkutano huo uliandaliwa na Naibu Waziri anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Dk. Abdalla Possi, pia ulihudhuliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aliye wakilishwa na Naibu wake, Bibi. Regina Kikuli na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu