Monday, December 28, 2015

MTU MMOJA AUWAWA NA MAJAMBAZI JIJINII DAR

Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Zantel (Head of customer care Zantel), Bw. Gabriel Kamukala ameuwawa kwa kupigwa na risasi eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam na watu waliodhaniwa ni majambazi baada ya kutaka kumpola pesa.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Zantel (Head of customer care Zantel), Bw. Gabriel Kamukala akiwa amedondoka chini baada ya kupigwa risasi. Habari zaidi zitafuata baadae.
Gari la marehemu likiwa eneo la tukio.
---
Kwa mujibu wa madirector wenzie waliofika pale eneo la tukio mara baada ya tukio kutokea... walinzi wakimasai wanasema jamaa walifika na boda boda wakapiga risasi kioo cha nyuma mmoja akamfata akawa anamwambia atoe hela... jamaa akachukua begi la laptop akawa anatoka nalo ndiyo vuta nikuvute jamaa wakampiga ya mkono... hakuachia...ndiyo wakampiga ya ubavuni ikaenda moja kwa moja kwenye mbavu...ndiyo iliyommaliza (kumuua)... Nasikia hiyo laptop ilikuwa zuga kana kwamba wamgechukua tu fasta bila kumdhuru wangekuta laptop tu... hela zimekutwa garini 10 milioni.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu