Monday, December 14, 2015

MWIGULU NCHEMBA AZURU ENEO LA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO MOROGORO

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Mwigulu Nchemba akiangalia mifugo iliyouwawa na wakulima.
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Mwigulu Nchemba, leo Desemba 14, 2015 ametembelea eneo palikozuka mapigano ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kujione uharibifu mbalimbali ikiwa ni kuuliwa kwa mifugo.

Kadhia hiyo iliyotokea kijiji cha Dihinda wilayani humo, tayari imepelekea kifo cha mwananchi mmoja huku askari polisi wawili na wananchi wengine wane wakijeruhiwa.

Waziri alishuhudia mifugo kadhaa iliyouwawa ikiwa imetapakaa kwenye eneo moja, hali kadhalika alitembelea hospitalini kuwapa pole majeruhi.

Akiongozana na Mbunge wa Mvomero Mh. Sadick Mourad, Mh. Waziri aliwataka wananchi hao kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Katika kujaribu kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo linalojirudia mara kwa mara, Mh. Waziri ameunda kamati za usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwa kila kijiji wilayani humo ambapo zitahusisha makundi yote mawili yaani wakulima na wafugaji ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua haraka iwezekanavyo. Waziri alifuatana na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu