Wednesday, December 9, 2015

OFISI YA WAZIRI MKUU YASHIRIKI KATIKA USAFI

Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakitekeleza agizo la Mhe.Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo la Ofisi ya Waziri Mkuu, Desemba 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifanya usafi wa mazingira Ofisini hapo Desemba 9, 2015 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe.Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la usafi wa Mazingira eneo la Magogoni Dar es Salaam tarehe 9 Desemba, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakitekeleza agizo la Mhe.Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo la Ofisi ya Waziri Mkuu, Desemba 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Ofisi ya Waziri Mkuu yaadhimisha siku ya Uhuru kwa Kufanya Usafi katika Eneo la Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani ( Ubungo Bus Terminal) na Eneo la Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maagizo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya kuadhimisha siku hiyo kwa Kufanya Usafi katika maeneo na mazimgira yanayotuzunguka.
Wakati wa Maadhimisho hayo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka aliwaeleza wafanyakazi wa ofisi hiyo pamoja na wananchi katika eneo la Stendi ya Mkoa kuwa kila wakati tufanye usafi na kwa kusimamia jambo hili litatusaidia kuepukana na magonjwa kama kipindupindu katika maeneo yetu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu