Friday, December 25, 2015

REBECCA MALOPE AWASILI NCHINI TAYARI KWA KUTOA BURUDANI DIAMOND JUBILEE X-MASS

1
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jioni hii tarayi kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Krismass litakalofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho likishirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa nchini Tanzania kama vile Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa na wengine wengi , kushoto katika picha anayefurahia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa na kumleta mwimbaji huyo Bw. Alex Msama.
2
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam, waliosimama nyuma Bw. Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Hadson Kamoga.
3
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA.
4
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na mmoja wa mashabiki wake kwenye uwanja wa ndege wa JNIA wakati alipowasili jijini Dar es salaam.
5
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na mratibu wa tamasha hilo Bw. Hadson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu