Wednesday, December 9, 2015

TBC, STARTIMES ZAKABIDHI MSAADA KWA MTOTO MWENYE ULEMAVU

Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Lanfang Liao (Kushoto) akimkabidhi Luninga Bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake mama mzazi wa Siraji Msuya, mtoto mwenye ulemavu Bi Mwajabu Yunusi (Kulia) kama mojawapo ya msaada kwa familia hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana ambapo naye kwa niaba ya shirika hilo alikabidhi Viti mwendo vinne, katoni tatu za pampasi pamoja na fedha taslim milioni tatu na laki tatu na sitini. Picha na mpiga picha wetu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Lanfang Liao (Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana na mama mzazi wa Siraji Msuya, mtoto mwenye ulemavu Bi Mwajabu Yunusi (Kulia) mara baada ya TBC na StarTimes kukabidhi msaada mama huyo baada ya taarifa inayomhusu mtoto huyo kutangazwa kupitia TBC1 siku za nyuma.   StarTimea ilitoa Luninga Bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake kama mojawapo ya msaada kwa familia hiyo, na TBC Ilikabidhi Viti mwendo vinne, katoni tatu za pampasi pamoja na fedha taslim milioni tatu na laki tatu na sitini. Picha na mpiga picha wetu.
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Lanfang Liao (Kushoto) akiteta jambo na mama mzazi wa Siraji Msuya, mtoto mwenye ulemavu Bi Mwajabu Yunusi (Kulia) mara baada ya kukabidhi  Luninga Bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake kama mojawapo ya msaada kwa familia hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana ambapo naye kwa niaba ya shirika hilo alikabidhi Viti mwendo vinne, katoni tatu za pampasi pamoja na fedha taslim milioni tatu na laki tatu na sitini. Picha na mpiga picha wetu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Lanfang Liao (Kushoto) akipeana mkono na mama mzazi wa Siraji Msuya, mtoto mwenye ulemavu Bi Mwajabu Yunusi (Kulia) mara baada ya kukabidhi  Luninga Bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake kama mojawapo ya msaada kwa familia hiyo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana ambapo naye kwa niaba ya shirika hilo alikabidhi Viti mwendo vinne, katoni tatu za pampasi pamoja na fedha taslim milioni tatu na laki tatu na sitini. Picha na mpiga picha wetu.
---
Na Mwandishi Wetu,

Shirika la Utangazaji la Taifa lijulikanalo kama Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) na kampuni ya urushaji wa matangazo ya televisheni kidijitali nchini ya StarTimes, imekabidhi misaada mbalimbali kwa mtoto mlemavu Siraji Msuya, miaka 13 anaeshi eneo la Ubungo Kisiwani Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Bw. Clement Mshana jijini Dar es Salaam Ijumaa, alisema TBC imefanikiwa kukabidhi vitu mbalimbali pamoja na fedha vilivyotolewa na wananchi walioguswa na hali ya mtoto huyo baada ya taarifa za mtoto huyo kurushwa na TBC1 siku za nyuma.

“Baada ya kutangaza taarifa hii kupitia TBC1 juu ya matatizo ya mtoto Siraji Msuya, leo tunakabidhi Viti Mwendo vinne, TV bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake iliyotolewa na kampuni ya StarTimes, Katoni tatu za pampasi pamoja na fedha taslim shilingi milioni 3 na laki tatu na sitini elfu.

TBC inapenda kutoa shukrani kwa makampuni na watu binafsi walioguswa na tatizo la mtoto Siraji Msuya na nayaasa makampuni na watu wengine binafsi wazidi kujitokeza kuisaidia familia ya mtoto huyu ili iweze kumudu kumsaidia siku hadi siku,” alisema Bw. Mshana.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao akikabidhi msaada huo wa TV Bapa yenye inchi 40 na dikoda ndani yake alisema baada ya kupata taarifa toka TBC juu ya mtoto huyo yeye na kampuni yake waliguswa na wameona umuhimu wa kumchangia mtoto huyo na familia yake.

“Kama StarTimes, tunasera ya kuunga mkono shughuli za kijamii ili kupeleka mbele maendeleo ya jamii. TBC ikiwa ni shirika ambalo tunashirikiana kwa karibu walivyotupatia taarifa za juu ya mtoto Siraji Msuya, tukaguswa moja kwa moja na tukaamua kutoa msaada huu kama kampuni.

Luninga hii itawezesha kuona taarifa za habari na kuangalia burudani mbali mbali zinazoendelea ulimwenguni,” alisema Bw. Liao.

Alisema Luninga hiyo bapa yenye inchi 40 inavisimbuzi ndani yake vinavyomuwezesha mteja kuunganisha moja kwa moja na dishi au antenna ya kawaida na kuangalia vipindi mbali mbali vinavyopatikana katika chaneli zinarushwa na StarTimes.

Naye mama Mtoto wa Siraji Msuya, Mwajabu Yunusi alipongeza makampuni na watu binafsi waliojitokeza kumsaidia mwanae na kutoa pongezi rasmi kwa mtangazaji wa TBC Rahel Mhando kwa jitihada alizozifanya ya kutoa habari juu ya mtoto Siraji Msuya.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu