Sunday, December 27, 2015

TUMSHUKURU MUNGU KWA KUMALIZA MWAKA 2015

Haikuwa rahisi tangu tuianze Jumapili ya kwanza mwezi Januari hadi leo hii tunaifikia Jumapili ya mwisho katika mwaka huu 2015. 

Yapo mengi mema Mungu ametufanyia, yapo mengi magumu adui alitupitisha, mengine magumu Mungu aliruhusu yatupate ili tuimarike zaidi imani zetu kwa kuutafuta msaada na uso wake hasa pale tulipotaka kukengeuka maana anatupenda. 

Iko mishale mingi ilielekezwa kwetu lakini katika yote Bwana amekuwa ngome na ngao yetu, mlinzi, mwamba na mtetezi wetu, amekuwa jabali letu na kinga yetu. Hakutuacha tufanywe mateka kwa adui zetu, hata pale walipotaka kula nyama zetu, hakutuacha tuwe mawindo yao wabaya wetu. 

Kuishi kwetu hata leo ni kwasababu ya neema yake. Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi nafsi yangu na iseme sasa. 

Katika hayo yote jua lipo kusudi Mungu anataka tulitimize hivyo kabla hatujaingia 2016, tumwuulize Mungu anataka tusimame wapi ili tukitimiza kwa msimu mwingine ujao. Happy last Sunday of 2015.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu