Thursday, December 10, 2015

UTT-PID YAINGIA MAKUBALIANO NA WIZARA YA MAMBO YA NJE KWA DHUMUNI LA KUENDELEZA VIWANJA VINAVYOMILIKIWA NA WIZARA KATIKA BALOZI MBALIMBALI UGHAIBUNI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (kulia) pamoja na mtendaji mkuu wa UTT-PID Dr. Gration Kamugisha (kushoto) wakiweka sahihi mikataba ya makubaliano ya uendelezaji wa maeneo hayo yanayomilikiwa na wizara katika balozi mbalimbali ili yawe na manufaa kibiashara huku wakishuudiwa na wasaidizi wao.
Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wakishuhudia utiaji wa Sahihi katika mkataba wa Makubaliano hayo.
Wakibadilishana mikataba ya ushirikiano na makubaliano hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula (kulia) wakipeana mikono na na mtendaji mkuu wa UTT-PID Dr. Gration Kamugisha (kushoto) mara baada ya kumaliza zoezi la wakiweka sahihi mikataba ya makubaliano ya uendelezaji wa maeneo hayo yanayomilikiwa na wizara katika balozi mbalimbali ili yawe na manufaa kibiashara huku wakishuudiwa na wasaidizi wao.
Picha ya pamoja ya watumishi wa UTT-PID pamoja na Balozi Liberata Mulamula baada ya kutia sahihi Makubaliano hayo.
---
Katika makubaliano hayo UTT-PID kwa kutumia mitaji itakayopatikana kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo Hati Fungani, Miundombinu ya aina tofauti ikiwemo majengo ya biashara na ofisi za kisasa za Ubalozi itawekezwa katika maeneo hayo ya balozi zetu katika mataifa mbalimbali ili iweze kuwa moja ya vyanzo vya mapato vya Serikali ya Tanzania kupitia tozo za kodi zitakazopatikana kutoka kwa wapangaji wa kada tofauti katika uwekezaji huo.

Pia itapunguza gharama za uendeshaji wa balozi zetu na hata kwa nchi ambazo Serikali imelazimu kupanga kwa ajili ya ofisi za Ubalozi ikijumuisha kuokoa fedha nyingi zitokanazo na ulipaji wa kodi ya pango.

Akitolea mfano Katibu Mkuu Balozi Mulamula alisema kuna nchi ambazo wizara inalazimu kulipa kati ya USD 10,000 mpaka 15,000 kwa mwaka kwa ajili tu ya Pango la ubalozi. Kwa hiyo kwa uwekezaji kama huu siku za usoni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaokoa fedha nyingi ya bajeti ambayo inatumika kulipia pango hususani katika nchi ambazo hakuna majengo ya ubalozi yanayomilikiwa na Wizara.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu