Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa akizungumza na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakati alipotembelea bandarini hapo leo jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Wizara na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mbarawa alipokuwa akitoa maelekezo ya kazi katika ofisi za Meneja wa Bandari mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na Naibu wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Eng. Mshana (katikati) mara walipowasili kwenye ofisi za Shirika hilo.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akifafanua jambo wakati wa upokeaji wa taarifa ya utendaji kazi wa TRL.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Eng. Mshana (wa kwanza kushoto), akitoa taarifa ya changamoto zinazoikabili shirika hilo kwa Mhe. Waziri Mbarawa.
Waziri Mbarawa akisisitiza jambo alipokuwa akitoa
maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), jijini Dar es
Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara katika Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na kubaini uondoshwaji wa wa kontena 329 bila kulipiwa kodi ya zaidi ya sh.bilioni 12, Mawakala wa Forodha walifanya ukaguzi kuona kama kuna upotevu wa mapato na kubaini jumla ya kontena 11,884 na magari 2019 yalitolewa bila malipo.

Makontena hayo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61, DICD 491, JEFAG 1, 450, AZAM 295, PMM 779, AMI 4384, TRH 4,424 ambazo kodi yake ni zaidi ya sh.bilioni 47.

Magari 2019 yalitolewa bila kulipa kodi katika kampuni za TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SILVER 97, MASS 171, HESU 1359 na kuinyima nchi kodi yenye thamani ya zaidi ya tsh.bilioni moja (1).


Akizungumza na wafanyakazi wa Bandari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema wataendelea kuchukua hatua dhidi ya wale ambao wamehusika wakiwemo watumishi wanaoshiriki katika hujuma.


Wafanyakazi saba wa TPA wanashikiriwa na polisi kuhusiana na upotevu wa kontena hizo na kusababisha serikali kukosa mapato.

Waliotiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kukamatwa leo ni John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman na Benadeta Sangawe.

Wanaotafutwa kwa tuhuma za kusababisha upotevu wa kodi za serikali katika bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: