Monday, December 21, 2015

WASHINDI 16 WAPATIKANA KATIKA DROO YA AIRTEL MKWANJIKA


 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akiongea na moja ya  washindi kupitia simu ya mkononi wakati wa kuendesha droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Abdallah Hemed  na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (kulia).
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bwana Abdallah Hemed  na Meneja masoko wa Airtel bi Anethy Muga (kulia)

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mkwanjika  na kuwapata washindi 16 wa  siku nne za mwanzo.
Promosheni ya Airtel Mkwanjika imezinduliwa na Airtel wiki iliyopita ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake katika msimu huu wa siku kuu za mwisho wa mwaka na X-mass  ambapo jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa na kampuni hiyo kushindaniwa na wateja wake kama  zawadi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo Meneja Uhusiano
wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel Mkwanjika leo tumewanyakuwa washindi 16 wa siku nne za mwanzo ambapo kila siku ni washindi wanne na kila mmoja ataweza kujizolea hadi shilingi milioni moja katika boksi letu la Airtel Mkwanjika.

Mmbando aliwataja walioibuka washindi wa kuingia katika boksi la Airtel Mkwanjika kuwa Mama Masisimba ,  Abdallah S Rashid, Amani Maruma, Msafiri Saidi Ruwia , Hassani Hamis Suleyman na  Aida Asabwile Mwafi wakazi wa mkoa wa Dar, es  salaam. 

Carston Magoah na Godfrey Frank Kamota wakazi wa Morogoro, Hassan Ngakoma mkazi wa Manyara , Safari Aidaru mkazi wa Mbulu, Lupembe Massanja  kutoka Rufiji , Rachel Obedi Muhumu mkazi wa Moshi na Rodrique kimei  mkazi wa Msumbiji. Washindi hawa  watapigiwa simu na kupatiwa maelekezo zaidi jinsi ya kupata na kupoke zawadi zao.

Nae Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga alisema “Promosheni yetu imeanza kufanikiwa kwa kuwa tayari tumewapata wateja wetu 16 na tumeshaandaa jumla ya milioni 16 ilikila mmoja akishajizolea pesa kwenye sanduku la pesa papo hapo tutampatia pesa yake aliyokusanya kupitia Airtel Money ili akasherehekee sikukuu kwa furaha zaidi”.
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa kiwango chochote kwenye simu zao kuingia moja kwa moja kwenye droo ya siku na kupata nafasi ya kujishindia pesa taslimu.

Hakuna gharama ya ziada wala  malipo yeyote unaongeza salio kwa
kutumia vocha, huduma ya Airtel money au kununua vifurushi vya yatosha na kujishindia pesa kila siku” alisisitiza Muga.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu