Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Reach for Change (R4C) wametangaza washiriki 15 wenye vipaji vya ujasiriamali wa kijamii wamechaguliwa katika shindano la “Tigo Digital Change Makers’ ambapo washindi wawili watatangazwa wiki ijayo.

Shindano hili lilioanza Septemba, limepokea mamia ya maombi kutoka kwa washiriki wenye ubunifu wa kiteknologia katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, ukulima na afya kwa mujibu wa Afisa wa Huduma kwa Jamii wa Tigo, May Thomas

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salam leo, May amesema, wajasiriamali wa kidijitali 15 waliochaguliwa kila mmoja wao alileta suluhisho la kidijitali lenye ubunifu lilokusudia kuboresha maisha ya watoto nchini Tanzania, na ndio kigezo kilicho wafanya wafuzu kushiriki katika shindano hilo.

May alisema: wengi katika hawa waombaji fikra zao ubunifu zimeenda sambamba na mkakati wetu wa kuleta mabadiliko ya kidijitali maishani. Hali imesababisha changamoto kubwa katika zoezi la kuchagua washindimda,” alisema, huku akiongeza kuwa washindi hao wawili watapokea dola za kimarekani 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kutekeleza miradi yao.

Tigo na Reach for Change wameendesha shindano hili la Digital Change-Makers nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, ambapo wajasiriamila wa kijamii saba wameshinda fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi yao. Kwa mujibu wa May, miradi ya wajasiriamali wa kijamii hao saba kwa pamoja imesaidia ya zaidi ya watoto 10,000 nchini katika kipindi hicho.

Shindano la Tigo Digital –Makers lina malengo ya kuwaendeleza na kuwatia moyo wajasiriamali wa kijamii kutumia teknolojia za kidijitali kusuluhisha baadhi ya matatizo sugu nchini Tanzania
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: