Ndugu zangu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya rais wetu tokea mwezi sasa aapishwe na kuanza kazi, kikubwa nilichojifunza ni kuwa siku ya Alhamisi ndiyo siku yake ya bahati ambayo huitumia kufanya mambo yake ya msingi, Ukianza kufuatilia tokea ameapishwa mpaka leo mambo yote amekuwa akifanya siku ya Alhamis.

Alitangazwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilikuwa ni simu ya ALHAMISI ya tarehe 29 Oktoba 2015, aliapishwa ALHAMISI ya tarehe 5 Novemba, 2015. Wakati huo alimteua Waziri Mkuu siku ya ALHAMISI ya tarehe 19 Novemba 2015, na sasa ameteua Baraza la Mawaziri leo ALHAMISI ya tarehe 10 Desemba 2015. Hata Yesu aliwaaga wanafunzi wake na kula nao chakula na kuwaosha miguu ni ALHAMIS KUU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: