NIMESTAAFU

Mwaka 2010, nilipata heshima ya kuaminiwa na Madiwani wenzangu pamoja na wananchi kuwa Meya wa Kinondoni. Mwaka 2015, kwa hiari yangu niliamua Kustaafu na hivyo sitakuwa tena Meya wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Nashukuru kwa heshima hii na kwa pamoja tumeifikisha Kinondoni hapa ilipofika. Najua bado kuna changamoto lakini tumepiga hatua kubwa sana na kuifanya Kinondoni kuwa Manispaa bora TANZANIA katika maeneo mengi.

Tumeboresha sana Mapato toka 10 bln mpaka 50 bln zitakazokusanywa mwaka 2015/16; tumeweka nidhamu kubwa ya matumizi, zaidi ya 60% ya Mapato ya ndani yanatumika katika miradi ya maendeleo; tumeboresha sana huduma za jamii - Elimu na Afya; pia katika kupunguza msongamano tumejenga madaraja na barabara; tumejenga Masoko ya wafanyabiashara; Tumetoa na kutenga Mikopo kwa Vijana na wanawake zaidi ya 2bln; tumejenga Umoja, kuboresha michezo pamoja na kuwa na timu ya mpira wa miguu inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Katika kipindi hiki Kinondoni imebadilika na kuwatofauti sana. Kinondoni sasa inajulikana kwa mazuri TANZANIA na AFRIKA. Tumedhihirisha hayo kwa kupata tuzo na pesa TANZANIA NA AFRIKA. Naamini tutapata viongozi wazuri watakao yaendeleza mazuri na kuipeleka mbele zaidi Kinondoni.

Nawashukuru sana Wanakinondoni, Naibu Meya Songoro, Waheshimiwa Madiwani wote, Mkurugenzi Natty na Wafanyakazi wote wa Kinondoni kwa kushirikiana pamoja bila kujali tofauti za itikadi na kuifikisha Kinondoni ilipofika. 

Nimestaafu uongozi wa kuchaguliwa lakini bado kama mwana Kinondoni nitaendelea kusaidia utatuzi wa changamoto za Kinondoni kwa kadri nitakavyoweza. NAWATAKIA KILA LA HERI VIONGOZI WA KIPINDI HIKI CHA HAPA KAZI TU.

MUNGU IBARIKI KINONDONI
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: