Thursday, December 17, 2015

ZANTEL YAZINDUA OFA YA MSIMU WA SIKUKUU KWA WATEJA WAKE

pic-zantel
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin.
---
Kampuni ya simu ya Zantel leo imetangaza kuzindua ofa maalumu kwa ajili ya msimu wa sikukuku yenye lengo la kuwazawadia wateja wake muda wa maongezi bure na nyongeza ya asilimia 20% katika kila manunuzi ya vifurushi au muda wa maongezi wanayofanya kupitia huduma ya Ezypesa.

Ofa hii pia itamzawadia kila mteja wa Zantel anayefanya manunuzi ya muda wa maongezi usio chini ya shillingi elfu moja kuweza kupata dakika za bure za kupiga Zantel kwenda Zantel siku za mwisho wa wiki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema ofa hiyo ni maalumu kwa ajili ya msimu huu wa sikukuku yenye lengo la kukuza ubora wa huduma na kuwapa wateja fursa ya kufurahia huduma za mtandao huo.

“Katika msimu huu wa sikukuku tumewazawadia wateja wetu ofa hii maalumu ili iwasaidie kutumia kiasi kidogo katika kufanya mawasiliano na ndugu,jamaa na marafiki kwenye msimu huu wa kusherekea sikukuu’ alisema Janin.

Zantel kwa sasa imejikita zaidi katika kukuza na kuboresha huduma zake na kuhakikisha inaboresha maisha ya jamii ya watanzania.

“Zantel pia imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inawafikia wateja wake na pia kukidhi mahitaji yao ya kimawasiliano, kwa kuboresha huduma zake huku ikitoa ofa zaidi zenye kusisimua kwa mwaka 2016 ‘alisema Janin.

Ofa hii imezinduliwa leo, ikiwa ni wiki moja tu toka bodi ya wakurugenzi wa Zantel ilipotangaza kuzindua mtandao mpya wa 4G kwa Zanzibar pamoja na kuimarisha huduma za kimawasiliano za mtandao huo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu